Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amefurahishwa na kiwango
kilichoonyeshwa na wachezaji wake na kufanikiwa kufuzu kwa nusu fainali
ya Kombe la Mapinduzi.
Kopunovic ameiongoza Simba kushinda mechi tatu
mpaka sasa ukiwemo ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe
juzi katika hatua robo fainali.
Mserbia huyo alisema kwa sasa bado timu yake haijacheza katika kiwango anachotaka na hakuna mchezaji mwenye uhakika wa namba.
“Sipendi kusema nina kikosi cha kwanza hata mtu
akiniuliza swali hilo silifurahii mimi nina wachezaji 11 wanaoanza siyo
kikosi cha kwanza, hata hapa Simba nimewaambia hakuna anayemiliki
namba,” alisema Kopunovic.
Katika hatua nyingine Kopunovic alisema yuko tayari kumpa muda mshambuliaji wake Dan Sserunkuma na kumtaka ajitume zaidi.
“Sserunkuma ni mtu muhimu hapa Simba, lakini ili atambulike kama mshambuliaji mzuri ni lazima ufunge.
“Hata mimi nilikuwa mshambuliaji, nilikutana na
kipindi kigumu kama anachopitia Dan, lakini anatakiwa kupambana zaidi
athibitishe uwezo wake.
Chanzo:mwananchi
Chanzo:mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment