Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakimpongeza kipa wao (aliyebebwa), Said
Mohamed baada ya kupangua penalti mbili katika mchezo dhidi ya Azam
katika mechi ya Robo Fainali ya kombe la Mapinduzi, uliopigwa jana
katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mtibwa ilishinda kwa penalti 7-6.
Mtibwa Sugar na Polisi Zanzibar zimetinga nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwa mikwaju ya penalti.
Awali Polisi Zanzibar iliwaondoa mabingwa
watetezi KCCA ya Uganda kwa penalti 5- 4, wakati Mtibwa Sugar
iliiondosha azam kwa penalti 7-6.
Kwa matokeo hayo sasa Polisi itacheza na Simba
iliyofuzu kwa nusu fainali juzi baada ya kuibamiza Taifa Jang’ombe mabao
4- 0, wakati Mtibwa Sugar itacheza hatua hiyo na mshindi kati ya Yanga
na JKU iliyokuwa ikicheza jana usiku.
Katika mchezo wa awali Polisi na KCCA zilimaliza
dakika 90 bila kufungana na hivyo kwenda hatua ya penalti huku kipa wa
Polisi, Nasir Suleiman akiwa nyota katika hatua hiyo baada ya kupangua
mikwaju miwili ya KCCA na mmoja ukigonga nguzo ya juu na hivyo
kuisaidia timu yake kutinga nusu fainali.
Katika penalti hizo waliofunga kwa upande wa Polisi ni Daniel Joram, Mohamed Seif, Abdallah Mwalim,
Mohamed Kiburungo na Ally Khalid wakati waliokosa ni Suleiman Ally na Juma Mgunda.
KCCA waliofunga ni Tom Masiko, Ronnie Kiseka,
Mpiima Saka na Owen Kasule wakati waliokosa ni Ivan Niege, William
Gwadri na Simon Namwanja.
Katika robo fainali ya pili, Mtibwa Sugar na Azam zilimaliza dakika 90 kwa sare1- 1 na kulazimika mshindi kuamuliwa kwa penalti.
Mtibwa ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa
dakika ya 63 na Ally Shomari akipokea pasi ya Mussa Hassan ‘Mgosi’ kabla
ya Azam kusawazisha bao hilo kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 90
aliyemalizia krosi ya Abubakari Salum.
Timu hizo zilianza mechi hiyo taratibu na kujikuta
zikienda mapumziko bila kufungana na ziliporudi kipindi cha pili
zilionekana kushambuliana kwa zamu.
Waliofunga penalti kwa upande wa Mtibwa Sugar ni
Shabani Nditi, Henry Joseph, David Luhende, Vicent Barnabas, Mussa
Nampaka, Muzamil Yassin na Said Mkopi wakati aliyekosa ni Amme Ally.
Azam wafungaji ni Aggrey Morris, Didier
Kavumbagu, Erasto Nyoni, Brian Majwega, John Bocco, Pascal Wawa wakati
waliokosa ni Kipre Tchetche na Aishi Manula.
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment