Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mahakama ya Chake Chake Pemba
imewatia hatiani wafanyakazi wawili wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)
baada ya kufanya ubadhilifu wa Tshs 19.2milioni mali ya Shirika la
Umeme na kutakiwa kuzilipa fedha hizo .
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa
Fedha Omar Yussuf Mzee huko Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar wakati alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa jimbo
la Wawi Nassor Juma alipotaka kujua sababu zilizopekekea wafanyakazi
kufukuzwa kazini.
Amesema uongozi wa
(ZRB)umewafukuza wafanyakazi hao baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la
jinai (Wizi) kwa mujibu wa kifungu cha 84cha Sheria ya Utumishi wa Umma
ya mwaka 2011 na kanuni za Utumishi za mwaka 2002 kifungu 69 (3) na
kutakiwa kulipa fedha hizo pamoja na faini ndani yake kwa kipindi cha
miezi miwili.
Akizitaja sababu za kufunguzwa
Waziri Omar Yussuf amesema kwamba ni kosa la kula njama kinyume na
Sheria ya Namba 6 ya mwaka 2004 ya Sheria ya Zanzibar
Hata hivyo Waziri huyo amesema
sababu nyengine za kufukuzwa ni kutengeneza hati ya uongo kinyume na
kifungu 340 (d) (1) na kifungu cha 342(2) ya Sheria ya namba 6ya mwaka
2014 kwa Sheria ya Zanzibar.
Akijibu swali la nyongeza Waziri
huyo ameeleza kuwa fedha hizo zimeshaanza kulipwa na kuna muelekeo wa
kumaliza kwani muda waliopewa na Mahakama hiyo ni mfupi (miezi miwili).
Sambamba na hayo Mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wenye tabia kama hizo.
0 comments:
Post a Comment