Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Serikali ya awamu ya saba
imechukuwa hatuwa mbambali za kuimarisha huduma za Elimu, Afya,Majisafi
na salama pamoja na Makaazi ili kuleta ustawi mzuri kwa jamii.
Hayo yameeelezwza leo na Makamu
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwasilisha hutuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wapili wa Rais kwa
Mwaka wa Fedha 2015/2016 huko Chukwani katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema Serikali imeendelea
kuchukuwa hatuwa madhubuti ya kuimarisha na kuendeleza elimu ikiwemo
ujenzi wa Skuli na Madarasa mapya kwa Skuli za Maandalizi Msingi na
Sekondari, pamoja na Ununuzi wa Vitabu vya ziada katika Skuli mbali
mbali za Unguja na Pemba.
Balozi Seif amesema Serikali
itaendelea kuwajengea uwezo Walimu kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu
na mfupi kwa lengo la kuimarisha ubora wa Elimu inayotolewa Maskulini
humo.
Aidha amesema pia Serikali
itaendelea kuimarisha huduma za kinga na Tiba katika Hospitali na Vituo
vya Afya sambamab na kutowa Elimu ya Afya kwa Wananchi kwa lengo la
kujikinga na maradhi ya kuambukiza na yasioambukiza.
Hata hivyo amesema Serikali
imezifanyia matengenezo makubwa Hospitali na Vituo vya Afya na kujenga
Majengo mengine mapya Unguja na Pemba ikiwemo Wodi ya wagonjwa mahatuti
(ICU) na kitengo cha huduma za upasuwaji Vichwa na Uti waMgongo (Neuro
Surgical Unit) katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Vile vile Serikali imechukuwa
Madaktari na Wahudumu wengine wa Afya kwa kuwasomesha na kuwapatia
uzowefu kutokana na Nchi kwani hivi sasa inamadaktari wazalendo.
“Hivi sasa Nchi yetu inamadakatari wazalendo wapatao 44 na Madaktari Bingwa wazalendo 13”, amesema Balozi Seif .
Kutokana na hali hiyo Serikali
imesema kwamba imeshawapatia Madaktari wa Maradhi mbali mbali kwa lengo
la kuwahudumia Wananchi kwa kushirikiana na Nchi marafiki.
0 comments:
Post a Comment