Na Mwandishi, Wetu Zanzibar.
WAJUMBE
wa Kamati ya Wawakilishi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Zanzibar
jana wamefanya Uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) na Katibu wa Kamati hiyo.
Jumla
ya Wawakilishi 22 watokanao na CCM wamejitokeza kuomba nafasi mbali
mbali za uongozi zikiwemo Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi ambaye pia
ni Katibu wa Kamati ya Wawakilishi wote wa CCM pamoja na Wajumbe Watano
(5) wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Kati
ya hao (22), watatu (3) wanaomba nafasi ya Unadhimu ndani ya Baraza la
Wawakilishi na 19 wanaomba nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
kupitia Chombo hicho.
Akitangaza
Matokeo hayo Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amemtangaza Mh. Ali Salum Haji kuwa
mshindi wa nafasi ya Unadhimu ndani ya Chombo hicho kwa kupata kura 36
na kuwashinda wagombea wenzake wawili Mh.Ali Suleimani Ali (Shihata) 32
na Mh. Abdallah Ali Kombo aliyepata kura 10.
Kwa
upande wa nafasi tano za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
walioshinda ni Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, aliyepata kura 51, Mhe.
Issa Haji Ussi Gavu kura 36, Mhe. Mihayo Juma Nungha kura 24, Mh. Riziki
Pembe Juma 43 na Mh. Asha Abdallah Mussa kura 33.
Uchaguzi
huo umetokana na matakwa ya Ibara 106 (s) ya Katiba ya CCM , Toleo la
2012 inayoelekeza kuwa kila inapofika wakati wa Uchaguzi, Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM watachagua Katibu wa Kamati za
Wawakilishi wote wa Chama hicho (Mnadhimu).
Akifungua
Mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd uliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM,
Kisiwandui Zanzibar amewataka viongozi waliochaguliwa katika Uchaguzi
huo kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa
ujumla.
Amesema
CCM ni Chama imara chenye viongozi weledi na makini waliokomaa kisiasa
na fani mbali mbali za kiuchumi na kijamii hivyo viongozi
waliochaguliwa hawana budi kuwakilisha vyema wananchi.
Mkutano
huo ulitanguliwa na Risala ya Wajumbe wa Baraza la Wazee wa CCM
Zanzibar ambapo ilisisitiza suala la umoja na mshikamano miongoni mwa
viongozi na wanachama wa chama hicho.
Akisoma Risala hiyo, Katibu wa Baraza hilo, Bw. Waziri Mbwana
amewapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuchaguliwa na
wananchi kwa kura nyingi kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika
Machi 20 mwaka huu.
Risala
hiyo, imewataka viongozi hao kufanya ziara za mara kwa mara matawini
kwa lengo la kuibua na kutatua kero mbali mbali zinazowagusa wapiga
kura wao majimboni kwa muda mwafaka.
Aidha,
imewataka Wawakilishi hao kuvunja makundi pale yalipokuwepo na badala
yake waelekeze nguvu katika kuunda kundi moja lenye nguvu litakaloweza
kusimamia maslahi ya CCM kwa vitendo.
0 comments:
Post a Comment