Home » » 18 mbaroni Micheweni kwa kuhatarisha amani

18 mbaroni Micheweni kwa kuhatarisha amani

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linawashikilia zaidi ya watu 18 kwa tuhuma za kusababisha fujo na kutishia amani katika wilaya ya Micheweni Pemba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kutokea fujo katika kijiji cha Maziwa Ng’ombe Micheweni katika nyumba ya Sheha Asha Yussuf.
“Tunawashikilia wananchi 18 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuhatarisha amani katika kijiji cha Maziwa Ng’ombe.....uchunguzi unaendelea na watakaobainika watafikishwa mahakamani,” alisema Nassir.
Wiki mbili zilizopita wananchi wa kijiji cha Maziwa Ng’ombe waliivamia nyumba ya Sheha na kuanza kurusha mawe huku wakiharibu shamba lake la migomba kwa kuikata. Matukio yote hayo ni mfululizo wa vitendo vya hujuma katika Kisiwa cha Pemba ambavyo vimeitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) ikiwemo migomo
Chanzo Gazeti La Habari Leo

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa