Home » » Rais akemea unyanyasaji wa kiitikadi

Rais akemea unyanyasaji wa kiitikadi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo ya ushuhuda kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Maziwa Ng’ombe wilaya ya Micheweni Pemba, Asha Yussuf Hassan (katikati) aliyevunjiwa nyumba yake na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukatiwa migomba yake wakati alipomtembelea nyumbani kwake kuangalia maafa hayo jana. (Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wakuu wa mikoa na wilaya, kutekeleza majukumu yao na kamwe wasikubali kuona wananchi wananyanyaswa kwa misingi ya itikadi za kisiasa.
Dk Shein alisema hayo Shengejuu wakati alipopewa taarifa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman aliyekuwa akitoa maelezo kwa Rais kuhusu mfululizo wa matukio ya vitendo vya hujuma dhidi ya wananchi.
Alisema wakuu wa mikoa na wilaya, wanayo mamlaka makubwa ya kusimamia utendaji wa maeneo yao, kwa hivyo hawatakiwi kuona wananchi wananyanyaswa kwa tofauti za itikadi za kisiasa.
“Wakuu wa mikoa na wilaya nimewateua kwa ajili ya kuongoza na kusimamia misingi ya utawala bora...msikubali kuona wananchi wananyanyaswa kwa tofauti za itikadi za kisiasa tu,” alisema. Hata hivyo, aliwataka watendaji hao kuongoza kwa kufuata misingi ya haki wala wasimuonee mtu haya au kumuweka kizuizini kwa chuki.
Chanzo Gazeti La Habari Leo

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa