Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na
Msingi Zanzibar Bi Safia Ali Rijali akizindua rasmi mafunzo ya siku tatu ya
kilimo cha mbogamboga na matunda
yaliyoanza Jumatatu tarehe 17/07/2017 Skuli ya Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa
wa Kaskazini Pemba.
Bw. Omar Abubakar akielezea changamoto
mbalimbali zinazoweza kujiokeza kaika kilimo cha kibiashara cha mbogamboga na
matunda na jinsi ya kukabiliana nazo.
Bw. Omar Abubakar akionesha kwa vitendo
jinsi ya kuatika mbegu kitaalamu kwa matarajio
ya matokeo bora.
Bw. Omar Abubakar akionesha kwa vitendo
jinsi ya kupima masafa yatakayotumika kuandaa matuta ambayo yataunganishwa na
mipira maalumu ya umwagiliaji kwa njia ya matone.
Wanafunzi wa Skuli za Makangale, Mgogoni
na Mkia wa Ng’ombe wakiwa katika harakati za kuandaa matuta.
Picha zote na Ali Othman
0 comments:
Post a Comment