Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHEHA wa shehia ya Matale wilaya ya Chakechake Mkubwa
Hamad Hassan, akifungua mkutano wa wazi wa kutoa elimu ya katiba na umuhimu wa
wananchi kushiriki, katika utungaji wa sheria, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma
za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika skuli ya Chanjamjawiri
shehiani humo, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
MRATIBU wa mkutano wa wazi wa kuwaelewesha
wananchi, umuhimu wa kushiriki kwenye utungaji wa sheria na katiba, kwa
wananchi wa shehia ya Matale wilaya ya Chakechake Pemba, Khalfan Amour Mohamed na
kufanyika skuli ya Chanjamjawiri wilayani humo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WATENDAJI wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakifuatilia igizo lililoandaliwa na Kampuni ya
Jufe Film Production ya Wete, kikiongozwa na Mwinyi Mpeku, lililoelezwa umuhimu
wa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watoto wanaobakwa au kulawitiwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
BAADHI ya vijana na watoto wa shehia ya
Matale wilaya ya Chakechake, waliohudhuria mkutano wa wazi wa kuelezwa umuhimu
wa kushiriki kwenye utungaji wa sheria na katiba, ulioandaliwa na Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika skuli ya
Chanjamjawiri wilayani humo, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
WASANII wa kampuni Jufe Film Production ya Wete, wakiongozwa
na Mwinyi Mpeku (mwenye kofia nyekundu) wakifanya igizo, lenye kuonyesha
umuhimu wa wananchi kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria, mara watoto
wanapolawitiwa au kubakwa, igizo hilo linafanyika skuli ya Chanjamjawiri na
liliandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Peemba).
WASANII wa Kampuni wa Jufe Film Production ya
Wete, wakiwa pamoja na waandishi wa habari na watendaji wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiwa kwenye picha ya pamoja, mara baada
ya kumalizika kwa mkutano wa wazi wa kuwaeleza wananchi umuhimu wa kushiriki
katika utungaji wa katiba na sheria, uliofanyika skuli ya Chanjamjawiri, (Picha na hisani ya Jufe Film Production).
0 comments:
Post a Comment