Shule 3 zabuni mradi kujiinua kwenye Kiingereza, Sayansi na Hisabati
UFAULU mdogo wawanafunzi shuleni hasa kwa masomo ya Sayansi,Hisabati na Kiingereza ni changamoto kubwa inayozikabili shule nyingi visiwani Zanzibar.
Hali hiyo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikichangiwa na sababu mbalimbali ikiwamo uhaba wa walimu,vitabu na utoro wa wanafunzi.
Hivi karibuni umeanzishwa mradi waelimu ambao umeandaa masomo ya ziada ya Hisabati na Kiingereza kuanzia darasa la tano hadi kidato cha nne kwa wanafunzi wa shule ya Kijini na Mbuyu Tende Matemwe ambao wapo nyuma kielimu.
Lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanafundishwa zaidi masomo hayo kwa muda wa ziada ili kupandisha kiwango chao cha ufaulu katika masomo yao, hasa watoto wa kike.
Mradi huo, unatoa masomo ya ziada mara tatu kwa wiki.Muda huo kama utatumiwa vizuri kuna kila dalili ya kupata mafanikio kwa kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi wa shule hizo kuwa na ufahamu hata kufaulu vizuri katika mitihani yao.
Kampuni ya Pennyroyal ambayo imewekeza katika sekta ya utalii Mkoa wa Kaskazini Unguja, ndiyo iliyoanzisha mradi wa elimu ya masomo ya ziada kwa wanafunzi wa shule ya Kijini na Mbuyu Tende Matemwe, Zanzibar. Unalenga kuinua kiwango chao cha ufaulu wa wanafunzi hasa masomo ya Hisabati na Kiingereza.
Mradi huo wa elimu umeanza hivi karibuni, yaani Juni mwaka huu,lengo ni kuwafikia wanafunzi wa kuanzia darasa la tano hadi kidato cha nne wa shule hizo zilizopo wilaya ya Kaskazini A,Unguja.
Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimia, kampuni hiyo hivi karibuni ilikutana na wazazi,walezi na walimu wa shule hizo kujaribu kutafuta ufumbuzi wa mahudhurio duni ya wanafunzi.
Meneja wa mradi huo wa elimu Ali Hamad Suleiman kutoka Kampuni ya Pennyroyal aliwaomba wazazi hao kuwaruhusu watoto wao kwenda kusoma masomo ya ziada ili kuhakikisha kuwa wanapata urithi mzuri wa elimu maishani
Kwa mujibu wa meneja huyo, wataendelea kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu bora na kujihakikishia ajira baada ya kumaliza masomo yao.
Mradi huo ulipoanza anasema, wanafunzi walikuwa na mahudhurio mazuri, lakini kwa sasa yameshukahivyo ni vyema wazazi wahakikishe kuwa watoto wao wanahudhuria masomo hayo kikamilifu.
“Mradi huu ukizingatiwa utaweza kutoa wanafunzi bora katika shule za Mbuyu Tende na Kijini Matemwe,”alifafanua .
Kampuni hiyo, ilianzisha mradi huo baada ya kuona kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwa masomo ya Hisabati na Kiingereza kuwa wa chini ukilinganisha na masomo mengine.
Mradi huo ukifanikiwa unalengwa kuwa endelevu kuwawawezesha wanafunzi sio tu kufaulu ni pamoja na kutengeneza fursa za ajira baada ya kuhitimu masomo kwa sababu ya kuandaliwa vyema.
Kwa sababu ya asilimia kubwa ya wakazi wa kijiji hicho kuwa wafuasi wazuri wa dini zao hivyo mkazo zaidi wameuweka katika masomo ya dini na kuwataka wajitahidi kuhakikisha elimu ya dunia inapewa uzito unaostahili.
Ofisa Elimu wilaya ya Kaskazini A, Mshamara Chum Kombo akizungumzia mradi huo alisema kuwa, wazazi wanapaswa kufuatilia mwenendo wa watoto wao kielimu ili kuhakikisha kuwa mafanikio ya kielimu yanafikiwa.
Miongoni mwa hatua alizopendekeza ni pamoja na kuwapunguzia majukumu ya kufanya kazi majumbani hasa watoto wa kike ili kuhakikisha kuwa wanapata muda wa ziada kusoma masomo hayo.
“Somo la Kiingereza naHisabatini ya msingi katika mawasiliano pia katika utendaji wa kazi hivyo mkazo mkubwa umewekwa kwenye masomo hayo kwa sababu muda wa kawaida shuleni hautoshi,”alisema.
Watoto alisema kuwa, wanahitaji kuhimizwa wayashughulikie masomo huku wazazi wakitakiwa kuhakikisha kuwa wanafuatilia vyema mwenendo wa watoto wao shuleni.
“Tatizo kubwa la wazazi ni kwamba wakishampeleka mtoto shule huwa hawana habari ya kufuatilia baadhi hawajui hata mtoto anasoma darasa la ngapi. Kwa hiyo, tunapotarajia matokeo mazuri lazima juhudi zielekezwe katika maandalizi,”alisema.
WAZAZI WAZUNGUMZA
Khamis Simai Khamis ni miongoni mwa wazazi wa watoto walio katika mradi huo, alisema kuwa utawasadia sana watoto wake na kuna dalili ya mafanikio mazuri kwa sababu sasa watoto wake waliopo darasa la tano wameanza kumudu kuzungumza Kiingereza.
“Hili linatupa mabadiliko, lakini baadhi ya wazazi tunakatishana tamaa kwamsimamo kuwa elimu ya shule sio elimu.Na kwamba elimu pekee muhimu niile ya dini (madrasa) tu,”alisema mzazi huyo.
Khamis alisema, somo la Kiingereza naHisabati ni muhimu kwani kuna baadhi ya viongozi wa dini wanatoa mafundisho ya dini kwa lugha ya Kiingereza ili kufikisha ujumbe.
Aliwataka watu wauthamini vyema mradi huo kwani fursa hiyo hairudi nyuma na bila ya elimu fursa nyingi za kimaendeleo zitakosekana.
Aliwashauri wamiliki wa kampuni inayoendesha mradi huo pia kuwapatia chakula cha mchana wanafunzi mazingira ambayo anaamini yatachangia kupunguza tatizo la utoro wa wanafunzi shuleni hapo.
“Mtoto anakuja Shule kuanzia saa moja hadi saa kumi na moja jioni, kwa ajili ya masomo ya ziada huwa hawajala kitu.Hapa hali zetu za maisha ni duni.
Lakini utakapowekwa utaratibu wa kuwapatia chakula shuleni sina shaka ari zaidi ya kusoma itaibuliwa na mahudhurio yao yatakuwa mazuri.
Mzazi mwingine Patima Mcha Hassan aliipongeza kampuni hiyokwakuwaanzishia mradi huo hivyo watajitahidi kuwahimiza watoto wao wahudhuria shule na katika masomo ya ziada ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Aliwataka wazazi wenzake kushirikiana kupinga ajira za watoto kutokana na ukweli kuwa watoto wengi wa kijiji hicho wamejikita katika sekta ya uvuvi ikiwamo kupara samaki baharini, badala ya kuhakikisha wanahudhuria shule kwani maendeleo ya kijiji hicho kielimu ni duni ukilinganisha na vijijini vingine.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Mbuyu Tende, Simai Haji Mcha alisema, mradi huo umekuja muda mwafaka ili kuwawezesha wanafunzi wapate elimu na wanapomaliza masomo yao wawe katika mazingira ya kupata ajira kwa sababu ya elimu yao.
Alisema ufaulu wawanafunzi wa shule yake kwa somo la Hisabati na Kiingereza ni mdogo, lakini anaimani kupitia mradi huo kwani ufaulu wao utaongezeka.
Alisema kunabaadhi ya watoto wamekuwa wakitoroka masomo hivyo nimuhimu wazazi wahakikishe watoto wao wanahudhuria shule.
“Wanafunzi wanaufahamu mzuri, lakini wanahitaji msukumo. Ukisema unawaachia ndipo wanapokatisha masomo na kuzurura mitaani,”alisema.
Shule hiyo inawanafunzi 504 kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha pili. Idadi ya walimu wanaofundisha shuleni hapo ni 13.
WANAFUNZI
Tano Jabu, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Mbuyu Tende akizungumzia mradi huo,alisema kuwa tangu uanze ni muda mfupi tu, lakini wanafundishwa vizuri hata kuwaongezea ufahamu kwa somo la Kiingereza na Hisabati.
Alisema siku tatu kwa wiki walizopangiwa kwa masomo ya ziada hazitoshelezi, hivyo wanashauri ni vyema uongezwe hasa ikizingatiwa kuwa Novemba mwaka huu wanakabiliwa na mtihani wa taifa.
Kama hiyo haitoshi, pia wanahitaji muda wa ziada wa kufundishwa masomo mengine hasa ya sayansi ambayo kuna upungufu wa walimu shuleni hapo.
Matarajio yake alisema kuwa ni kufaulu vizuri mtihani na kufanya vizuri katika masomo yake shuleni hapo.
Nae Ummi Ali Makame, mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo, alisema siku chache tangu mradi huo uanze ameona mabadiliko katika elimu wanayopatiwa.
Masomo ya ziada alisema yamemwezesha sasa kuzungumza angalau kwa kujitambulisha na salamu kwa lugha ya Kiingereza wakati mwanzoni hakuwa akifahamu kabisa.
“Hata somo la Hisabati nilikuwa naliona gumu lakini sasa nalipenda na mwalimu anapofundisha huwa namsikiliza kwa umakini mkubwa,”alisema.
Kuhusu utoro wa wanafunzi alisema upo, lakini umekuwa ukisababishwa na baadhi ya wazazi na walezi wa watoto ambao wanawapa majukumu mazito watoto wao hata kuchangia kuwafanya washindwe kuhudhuria shule na kukosa masomo.
“Baadhi ya wazazi huwapa mifugo watoto wakachunge mbuzi au ng’ombe bila ya kujali kuwa huo ni muda wa shule au vipi,”alisema.
Pia baadhi ya watoto wamejikita katika shughuli ya uvuvi ikiwamo kwenda pwani kupara samaki ili kupata fedha.za kujikimu
Hayo yote alisema, yanatokana na hali ya umaskini kwa sababu baadhi ya wazazi huwategemea watoto wao wanapofanya kazi hizo kuwapatia fedha zinazochangia kutatua changamoto mbalimbali za kifamilia.
Chanzo:Nipashe

0 comments:
Post a Comment