Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo
Mh. Khatibu Juma Mjaja akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa
Habari na Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini
kwake Chake Chake Pemba.
Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Maalim Suleiman Amour
Suleiman akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na
Mahusiano wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Ali Othman Ali Ofisini kwake Chake
Chake Pemba.
Na Ali O. Ali
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo
Mh. Khatibu Juma Mjaja ameelezea matumaini
yake ya mafanikio katika sekta ya utalii kisiwani Pemba kupitia tamasha la
michezo na utamaduni lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki Network.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti cha shukrani
Ofisisni kwake Chake Chake Bwana Mjaja amesema Rafiki Network imefungua njia
katika kuimarisha utalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na kuandaa na
kusimamia Tamasha la kimichezo liloandaliwa kwa ubunifu na ustadi huku
likijumuisha michezo mbali mbali ya asili ambayo niburudani kwa wenyeji na
kivutio kwa wageni.
Mh. Mjaja ameuomba uongozi wa Taasisi ya Rafiki Network
kuhakikisha kwamba Tamasha hili linakua endelevu ambapo amebainisha kwamba
kuendelea kwa tamasha hilo kila mwaka kutasaidia kukuza hali za watu katika
Nyanja mbali mbali kiuchu na kiutamaduni.
Akifafanua ubunifu uliofanyika katika maandalizi ya Tamasha
la kimichezo Kisiswani Pemba, Mh. Mjaja amesifu uteuzi na mpangilio wa barabara
zilizotumika katika mchezo wa mbio za Baiskeli nakuongeza kwamba mpangilio huo
uliwapa fursa wananchi waliowengi kuweza kushiriki kikamilifu katika michezo
mbali mbali. Afisa huyo pia amewapongeza Azam TV kwa kurusha matangazo ya moja
kwa moja ya Bonanza hilo.
Nae Afisa Mdhamini Kamisheni ya Utalii Pemba Maalim Suleiman
Amour Suleiman amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network
kutokana na mchango wake mkubwa katika kufanikisha Tamasha hilo.
Taasisi ya Rafiki Network iliandaa Tamasha la kimichezo
Kisiwani Pemba mnamo Julai 28-30 ambalo lilijumuisha michezo mbali mbali ikiwa
ni pamoja na mchezo wa Ng’ombe, Mashindano ya Baiskeli, Mashindano ya kuogelea na Resi za Ngalawa.
0 comments:
Post a Comment