Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Timu za Soka wilaya ya Magharibi A Unguja zimetakiwa kufika katika ofisi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) za Wilaya ya Magharibi A Unguja hiyo ili kukamilisha masuala mbali mbali yanayohusiana usajili wao kabla ya Agosti 31, 2015.
Katibu Mkuu wa ZFA Zainab Omar Mussa ameeleza kuwa pamoja na kukamilika kwa zoezi la usajili ameona haja ya kutoa muda huo ili kutoa nafasi kwa timu hizo kusawazisha dosari katika fomu zao sambamba na kukamilisha malipo ya baadhi ya ada zinazostahiki.
Zainab ameeleza kuwa zoezi hilo katika wilaya hiyo lilienda vyema na kwamba klabu hizo zinatakiwa a kufanya marekebisho hayo kabla ya Kamati Tendaji kukutana na kuzipitia fomu hizo mwanzoni mwa mwezi ujao.
Katibu Zainab ameeleza kuwa katika kipindi cha usajili kilichoanzia Julai 17 - Agosti 17, 2017 timu 35 zilichukua fomu za usajili wa kushiriki mashindano ya ligi daraja la pili na tatu katika msimu ujao.
Msimu wa 2017/18 utakuwa ni wa pili toka kuasisiwa kwa ZFA hiyo mwishoni mwa mwaka 2015 naada ya kugawanywa kwa iliyokuwa wilaya ya Magharibi, Unguja ambapo katika msimu uliopita klabu 30 zilishiriki ligi daraja la pili wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment