Raia
wa Ujerumani Gerd Winkdl (60), amefariki dunia Zanzibar akidaiwa
kuchomwa kisu na marafiki zake wa kike kutokana na wivu wa kimapenzi
huku wanawake wanne wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo
hicho.
Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo lilitokea
majira ya saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa
na marafiki zake hao.
Alisema
kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao
wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye
ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili
wake.
Kamanda
Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa
Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya
kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.
"Inasemekana
wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi ni wivu wa
kimapenzi, lakini tunaendelea na uchunguzi," Kamanda huyo alisema.
Aidha, Kamanda Ali alibainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mnazimmoja kisiwani hapa.
Aliongeza
kuwa raia huyo wa kigeni alikuwa anaishi Zanzibar akiwa ni msimamizi wa
mapishi katika hoteli moja ya kitalii kisiwani hapa.
0 comments:
Post a Comment