
.
Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya
kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao.
Hayo
yamesema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati
akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe,
Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya
sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.
“Katika
Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali
hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa
muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja
hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki
wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti
za Busara, Yusuf Mahmoud.
Anaongeza
kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee
huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya
kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya
maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu
wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata
zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.” Likisifika kuwa miongoni mwa
matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya
“Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya
wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar.
Likiwa
ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake
na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na
muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine,
ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki
kuutanganza muziki wao duniani.
“Kila
mwaka, kila mwanamuziki anayepata fursa ya kutumbuiza katika jukwaa la
Sauti za Busara, hualikwa kuzunguka katika miji mbalimbali duniani na
kufanya maonesho kwenye matamasha yanayofanyika katika nchi hizo.
Wanamuziki
ambao hupata fursa ya kualikwa aghalabu, ni wale ambao wamethibitika
katika maonesho yao kuwa wabunifu, wenye kuzungumza ujumbe fulani, na
wanaocheza muziki wenye utambulisho fulani,” anasema Yusuf, akiwataja
Msafiri Zawose, Jagwa Music, Leo Mkanyia, Tausi Women’s Taarab na
Maulidi ya Homu ya Mtendeni kama mifano ya vikundi vya Kitanzania
ambavyo tayari vimekwishaitwa katika safari za kimataifa baada ya
kuonekana katika Tamasha la Sauti za Busara.
Kulingana
na maelezo ya Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud,
Tamasha la Sauti za Busara ni fursa adhimu ambayo wanamuziki kutoka
Tanzania hawatakiwi kukosa, kwa kuwa fursa kama hizi ni chache na ngumu
kuzipata ndani ya Afrika.
“Watu
wa rangi tofauti huungana kwa pamoja kusheherekea muziki wa Kiafrika.
Matarajio na msisimko ni mkubwa, hoteli zinazopatikana Stone Town huwa
zinajaa katika wiki ya tamasha zikiwahudumia watu wanaotoka katika kila
kona ya Tanzania, Afrika na Ulaya,” anasema Yusuf. Kwa makadirio ya
haraka, tamasha linachangia kiasi cha Dola za Marekani 7 milioni katika
uchumi kila mwaka, kikiwa ni kipindi cha mavuno kwa biashara nyingi
zinazofanyika kwenye kila pembe ya Zanzibar na sehemu zingine, na
kulifanya Tamasha la Sauti za Busara kuwa zaidi ya ‘Tamasha la Muziki’.
Hata
hivyo, licha ya kuwa na mafanikio hayo yote, lakini changamoto kubwa
inayolikumba tamasha hili ni ufadhili, na ndiyo sababu hata tamasha la
mwaka 2016 lilifutwa na kusababisha hasara kubwa sana kwa biashara
nyingi visiwani Zanzibar. “Tunaendelea kutegemea fedha za wafadhili
kutoka katika balozi mbalimbali, ambapo balozi za Norway na Uswisi
zikiwa miongoni mwa wafadhili wakubwa, zikisaidia mafunzo na jitihada za
ujengaji uwezo,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,
Yusuf Mahmoud.
Tamasha
la Sauti za Busara 2018 linafadhiliwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa
Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Africalia, Mozeti, Zanlink, Memories
of Zanzibar, Zenj FM, Chuchu FM, Tifu TV, Music In Africa, Ikala
Zanzibar Stone Town Lodge, Emerson Zanzibar, Coastal Aviation, 2Tech
Security, Ubalozi wa Ujerumani, Golden Tulip Dar City Centre.
0 comments:
Post a Comment