Afisa Uhamiaji Ndg. Ali S. Nasor Mkuu wa Utawala na Fedha (DCI) Makao
Makuu ya Ofisi ya Uhamiji ZanzIbar akiweka saini kwenye kitabu cha
wageni alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho
(NIDA) viwanja vya Maisara - Unguja.
Wananchi
waliotembelea Banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) wakifuatilia Vitambulisho vyao kutoka Shehia mbali mbali za Mjini
Unguja, wakati zoezi la Ugawaji Vitambulisho likiendelea.
Mamia
ya wananchi wa Tanzania Zanzibar wameendelea kufurika katika viwanja
vya Maisara Zanzibar kunakofanyika Tamasha la Nne la Maonyesho ya
Biashara la Zanzibar; yakiwa ni sehemuu ya maadhimisho ya miaka 54 ya
Mapinduzi Zanzibar.
Katika
maonyesho hayo pamoja na mambo Mengine Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa inatoa huduma ya ugawaji Vitambulisho vya Taifa, kusajiliwa kwa
wale ambao hawakuwahi kusajiliwa pamoja na kupatiwa maelezo yanayohusu
huduma zinazotolewa na Mamlaka.
Miongoni
mwa Shehia ambazo Vitambulisho vinatolewa ni Mkunazini, Kiponda,
Shangani,Kikwajuni juu, Kikwajuni Bondeni,Kisima Majongoo,Kiswandui,
Malindi, Mchangani,Mwembe Tanga, Kilimani, Urusi, na Jang’ombe,.
Akizungummzia
huduma zinazotolewa kwenye Banda hilo Meneja wa Mifumo wa Komputa ndugu
Abdallah Mmanga amesema Wananchi waliofika kwenye Banda la NIDA
kusajiliwa wanatakiwa kufika na nakala ya Cheti cha kuzaliwa, Vyeti vya
shule kuanzia na Cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi, Pasi ya kusafiria
(Pasport),Kadi ya Kupigia kura, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi,
Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya mfuko wa Jamii
(NSSF,ZSSF,PPF,GEPF nk)
Pindi
maonyesho hayo yatakapomalizika; wananchi ambao watakosa fursa
wameshauriwa kufika kwenye ofisi za NIDA zilizopo kwenye kila Wilaya kwa
Unguja na Pemba; ili kusajiliwa pamoja na kuendelea kuchukua
Vitambulisho vyao kwa wale ambao wamekamilisha taratibu za Usajili.
Kwasasa
Zanzibar imekamilisha Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa kwa
asilimia 99 na mipango ya kuanza rasmi kwa matumizi ya Vitambulisho vya
Taifa inaendelea kupitia wadau mbalimbali ili wananchi kuanza kunufaika.
0 comments:
Post a Comment