Home » » Brigedia Adam Mwakanjuki afariki Dunia

Brigedia Adam Mwakanjuki afariki Dunia

liyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu wamesema kwamba taarifa ya mazishi itatolewa leo baada ya kukutana wanafamilia hiyo visiwani Zanzibar.
“Ni kweli Mjomba amefariki hivi punde dare s salaam na mipango ya mazishi itapangwa baada ya kikao cha familia yetu” alisema Vicky Mwakanjuki mtoto wa Dada wa Marehemu.
Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.

Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa