Jumla ya shs Billioni 71 wamejipatia Wakulima wa Zao la Karafuu
Kisiwani Pemba baada ya kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar
(ZSTC) Karafuu zao zao katika msimu wa Karafuu unaotarajiwa kumalizika
hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dkt Ali
Mohamed Shein ameyaeleza hayo leo hapo katika ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi alipokuwa akitowa shukrani kwa Viongozi mbali mbali wa Mkoa
huo wakiwamo vikosi vya ulinzi vya Polisi, JKU,KMKM,,ZIMAMOTO,VALANTIA,
MAFUNZO,MASHEHA, WANANCHI NA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA USIMAMIZI WA
ZAO LA KARAFUU ZANZIBAR.
Amesema kuwa kiasi hicho cha Fedha kimo mikononi mwa Wananchi
ambapo kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwasaidia sana katika maendeleo yao.
Dkt Shein amefurahishwa na juhudi mbali mbali mbali za Maendleo
zinazochukuliwa na Wakulima kwa kuweza kujenga Nyumba za Kisasa baada
yakupata Fedha hizo za Karafuu ambapo pia amewataka kuchukuwa kila
juhudi yakusafisha Mashamba yao na kupanda Mikarafuu mipya.
Aidha Dkt Shein amefurahishwa na juhudi ya pamoja ziliochukuliwa na
Viongozi mbali mbali, Wananchi, Masheha pamoja na Vikosi vya Ulinzi
katika kuhakikisha kuwa msimu huu zao la Karafuu halitoroshwi kwa njia
ya Magendo.
Amesema kuwa kosa juhudi za pamoja mafanikio hayo yasingeweza
kupatikana ambapo mwaka jana Mkoa wa Kaskazini Pemba ZSTC ilinunuwa
jumla ya Tani 25 .6 tu wakati msimu huo katika Mkoa huo jumla ya tani
2180.5 za Karafuu zimenunuliwa.
Ameeleza kuwa kutokana na kazi nzuri iliofanywa safari hii hakuna
hata Mkulima moja ,wala taasisi za binafsi na Serikali ambazo inalidai
Fedha Shihirika la Taifa ZSTC.
Hata hivyo aliliagiza Shirika la ZSTC kuziangali changamoto
zilizojitokeza katika msimu huu na baadae kuzipatia ufumbuzi ili msimu
ujao uweze kwenda vizuri zaidi
Changamoto hizo ni kwa Vituo vya kununuwa Karafuu kujitosheleza
katika hali zote zikiwamo sehemu za kujisaidia ,Vifaa vya kukalia na
pia kuweka Umeme katika vituo.
Mapema Dkt Shein amesema kuwa kwa upande wa Serikali itajitahidi
katika kutengeneza Barabara za Vijijini ili zao hilo na mengine
yaweze kupita bila ya matatizo na kusisitiza kuwa vita dhidi ya Magendo
ya Karafuu ni lazima kwa Wananchi kuendelea kupiga vita ili nchi izidi
kufaidika kwa zao hilo am,balo ni tegemeo kwa Uchumi wa Nchi na Taifa
kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment