Home » » Sekta binafsi visiwani Zanzibar yataka gharama za uendeshaji biashara za umeme ziwe nafuu, ili kuwepo na huduma za uhakika

Sekta binafsi visiwani Zanzibar yataka gharama za uendeshaji biashara za umeme ziwe nafuu, ili kuwepo na huduma za uhakika



Sekta binafsi visiwani Zanzibar imelalamikia ongezeko la gharama za umeme kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na gharama za Tanzania Bara. Pamoja na hilo, nishati hiyo bado pia imekua sio ya uhakika kutokana na miundombinu yake ya usambazaji kuwa mibovu.



Katika mkutano uliofanyika baina ya sekta binafsi na sekta ya umma ulioongozwa na Shirika la Kitaifa la Zanzibar la Biashara, Viwanda na Kilimo (ZNCCIA), imebainika kuwa gharama kubwa za umeme na upatikanaji wake usiokuwa wa uhakika ni kikwazo kikubwa kinachozuia uboreshaji wa mazingira ya biashara visiwani humo.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa ZNCCIA, Bw. Ali Aboud na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bi. Munira Hamoud, walisema, gharama kubwa za nishati ya umeme sio tu kuwa zinawaumiza watumiaji wa kawaida bali pia zinaweza kuzorotesha uzalishaji viwandani.

Viongozi hao pia walibainisha kuwa kuongezeka kwa gharama hizo za umeme kutasababisha mfumuko wa bei visiwani humo na hivyo kusababisha kuongezeka kwa gharama za kuendeshea biashara.

Dk. Mohammed Hafidh Khalfan, ni mwanauchumi maarufu, ambaye amepewa jukumu na ZNCCIA chini ya programu ya BEST-AC kuangalia masuala hayo alisema:

“Gharama za umeme ndio kikwazo kikubwa cha mendeleo ya biashara, uendeshaji na ukuaji wake visiwani Zanzibar. Bila kuwa na suluhisho la kudumu la kutatua kikwazo hiki, ndoto ya Zanzibar ya kuwa na uchumi wa tabaka la kati ifikapo mwaka 2020 haitafikiwa, badala yake hali itakuzidi kuwa mbaya. "

Dk. Khalfan ametoa maoni yake kuwa Zanzibar ina uwezo wa kuvutia uwekezaji mkubwa lakini gharama za uzalishaji zinazosababishwa na tatizo la umeme miongoni mwa matatizo mengine, limepoteza matumaini ya kuweza kuyafikia malengo yaliyobainishwa katika Sera ya Uwekezaji ya Zanzibar.

 “Athari za gharama kubwa za umeme zinaweza kukisiwa na kupata picha halisi: gharama kubwa za umeme huchangia kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, na pia hupunguza uzalishaji na faida kwa mfanyabiashara," alisema

Gharama mpya za umeme.

Shirika la Umeme visiwani Zanzibar (ZECO) kuanzia tarehe 1 Juni mwaka huu liliongeza bei za umeme kama ifuatavyo: gharama kwa watumiaji wa kawaida (ikiwa ni pamoja na watumiaji.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa