Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kauli hiyo ilitolewa jana katika mkutano wa hadhara wa jumuiya hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Binti Amran mjini Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alisema
kimsingi hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinatakiwa kufanya kazi
kwa bidii, ushirikiano na umakini mkubwa ili kuvitokomeza vitendo hivyo
mara moja.
Aliviomba vikosi hivyo kujenga umakini na ushirikiano wa karibu
katika kipindi hiki kigumu kuliko wakati wowote ili kufanya kazi kwa
pamoja na kuibaini mitandao ya kihalifu katika ukanda mzima wa Afrika
Mashariki.
Hata hivyo, alizitaka Serikali mbili za Muungano na
Zanzibar kuwakabili na kuwaasa viongozi wanaochanganya dini na siasa na
kueleza kuwa jambo hilo likiachiwa linaweza kuzaa matatizo yatakayoleta
madhara makubwa.
Alitolea mfano mataifa ya Syria, Nigeria, Somalia, Iraq, Misri na
Jamhuri ya Afrika ya Kati kama yanayotatizwa hivi sasa kutokana na watu
wake kutaabika, kupoteza maisha, huku watoto na wanawake wakihangaika.
Alisema kitendo cha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
si tiketi itakayomsaidia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
kushinda urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment