Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi
Alitoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ma-RC na ma-RAS kutoka mikoa yote nchini, jana jijini Dar es Salaam.
Balozi Iddi alisema kumekuwapo changamoto ya mahusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala na kuwasababisha baadhi yao kuamua kufanya kama wanavyoona.
Alisema misuguano hiyo imewafanya baadhi ya viongozi kupeleka malalamiko ama kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) au Katibu Mkuu Tamisemi.
“Ninyi viongozi, ambao mmekabidhiwa dhamana kubwa katika mikoa yenu, ambako ndiko Watanzania wote wanaishi, ndiyo wawakilishi wa Rais. Uwajibikaji na mshikamano wenu ndiyo sababu pekee itakayowezesha Watanzania kuboresha maisha yao,” alisema Balozi Iddi.
Aliongeza: “Kumekuwa na changamaoto ya mahusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa. Hali hii imesababisha baadhi yenu kuamua kufanya anavyoona kwake inafaa.”
Alisema wakuu wa mikoa ni viongozi wa kisiasa, huku makatibu tawala wa mikoa wakiwa ni watendaji wakuu kwenye ngazi hiyo, hivyo akataka kuwapo uwazi wa mawasiliano baina yao, mshikamano, kuacha kushikilia misimamo na kutekeleza majukumu yao kwa muingiliano.
Pia aliitataka Taasisi ya Uongozi nchini, ambayo ndiyo waratibu wakuu wa mafunzo hayo, kuandaa mafunzo mengine ya jinsi hiyo kwa ajili ya wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya pamoja na wakurugenzi wao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alisema mafunzo hayo yanalenga kuimarisha mawasiliano, mahusiano na muingiliano baina ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa pamoja na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mafunzo hayo ni kwa ajili ya mikoa yote nchini, lakini ni mikoa 20 pekee hadi jana ndiyo iliyothibitisha kuwapo, huku mingine ikiwa na udhuru maalumu.
Alisema mikoa ambayo haikuhudhuria kwa upande wa Tanzania Bara itashiriki katika mafunzo mengine yatakayotolewa hivi karibuni kwa upande wa Zanzibar.
Aliungana na Balozi Iddi kuwataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuheshimiana kwa kuwa kila mmoja ana nafasi yake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment