Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi Seif, alieleza hayo wakati akiuzindua rasmi mpango maalumu
ulioandaliwa kwa pamoja kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar
(ZSSF), na Benki ya Posta Tanzania (TPB), wa ukopeshaji uliolenga kwa
wafanyakazi wastaafu wa ZSSF, hafla iliyofanyika ukumbi wa hoteli ya
Ocean View, Kilimani mjini hapa.
Mikopo hiyo inayotolewa na TPB kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar, huwasaidia wastaafu kulipia gharama za matibabu, ada za shule
kwa familia zao sambamba na kuendesha biashara ndogo ndogo
zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Balozi Seif alibainisha kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ni kujenga mazingira mazuri kwa wastaafu wake, ili kustaafu
kwao kusiogopwe na kuonekana ni mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha maisha
ya shida yasiyokuwa na matumaini.
Alisema serikali inataka kuona wafanyakazi wake wanapopata barua za
kustaafu, wasianze kuhuzunika kama ilivyozoeleka, kwa vile wengi kati
yao huhisi kwamba wamefika wakati ambao hawawezi kukopesheka tena
kutokana na udogo wa mapato yao wanayopewa kupitia pensheni zao.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema kwa muda
mrefu sasa taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini zimekuwa hazitoi
mikopo kwa wastaafu kwa dhana kwamba hawana uwezo wa kuirudisha.
Moshingi alisema Benki ya Posta kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii Zanzibar, ililiona tatizo hilo baada ya kutambua mchango mkubwa
uliotolewa na wastaafu hao wakati wa utumishi wao na kufikia uamuzi wa
kubuni mpango huo ambao ni mkombozi kwa wastaafu hao.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF, Khamis Filfil Thani,
alisema mafao ya wastaafu muda mwingi huongeza mapato ya taasisi za
fedha na kuleta utulivu kwa wastaafu.
Alieleza kwamba mzunguko wa mafao ya wastaafu katika taasisi
mbalimbali za kifedha nchini, umefikia sh trilioni 2 wakati ule
unaosimamiwa na ZSSF uliohusisha wastaafu 4,000 umefikia sh bilioni 20.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment