Home » » TAHLISO YACHARUKIA WANASIASA

TAHLISO YACHARUKIA WANASIASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu Mwenyekiti wa Tahliso, Abdi Muhamoud Abdi
JUMUIYA ya Vyuo Vikuu Tanzania (Tahliso), imekemea vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa nchini kutumia Serikali za wanafunzi wa vyuo hivyo kutoa matamko ya kuwaunga mkono katika hatakati zao za kisiasa.
Onyo hilo lilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tahliso, Abdi Muhamoud Abdi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar jana.
Alisema imekuwa ni kawaida ya viongozi wa siasa kuwatumia wanafunzi wa vyuo vikuu katika majukwaa ya kisiasa, jambo ambalo katiba yao hairuhusu kiongozi wa Tahliso kupanda katika majukwaa ya kisisa na kujinadi kupitia jumuiya hiyo.
“Kwa mujibu wa katiba ya Tahliso ibara ya 5 (2), ni marufuku kwa kiongozi yeyote hasa wa ngazi ya juu kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa hasa kupanda jukwaani, kwani kufanya hivyo ni kuiwakilisha taasisi katika siasa wakati ni ya kijamii,”alisema.
Kwa mujibu wa Mahmoud, Aprili 3 mwaka huu, katika kikao cha Seneti cha Tahliso kilichokutana jijini Dar es Salaam, kiliamua kumuondoa madarakani Musa Mdede kutokana na kwenda kinyume na katiba hiyo.


“Cha kushangaza baada ya miezi sita kupita na uongozi kubadilika katika serikali za wanafunzi wa vyuo mbalimbali, Mdede alitisha kikao na kuwadanganya viongozi wapya akiendelea kujitangaza kama mwenyekiti wa Tahliso,”alisema Mahmoud.
CHANZO:TANZANIA DAIMA

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa