Home » » MFUMO WA BARABARA ZANZIBAR WAZINDULIWA

MFUMO WA BARABARA ZANZIBAR WAZINDULIWA

Na Nafisa Madai  
Waziri
wa miondombinu na mawasiliano Hamad Masoud Hamadi amesema kuwepo kwa
mfumo wa uendeshaji wa matengenezo ya barabara (road maintenance
management system) RMMS, kutasaidia katika kutayarisha bajeti kulingana
na mahitaji  ya matengenezo hayo.
Amesema hayo wakati alipokua akizindua rasmi mfumo huo  ambao  utakua na mafanikio makubwa  katika kuonyesha aina ya barabara zinazohitaji kupewa kipaumbele katika matengenezo.
Hata
hivyo alisema iwapo taratibu zote zitafuatwa za mfumo huo kuna faida
nyingi zinaweza kupatikana ikiwa pamoja na kuweza kupata taarifa nyingi
zinazohusiana na mtandao wa barabara  kama vile ukubwa wa barabra,thamani yake pamoja na ubora wa barabara hizo.
Aidha utao toa taarifa sahihi za jina la barabara,urefu,upana, alama  katika barabara , kalvat  pamoja na madaraja.Pia utaweza kukadiria gharama za matengenezo ya barabara husika.
Sambamba na hayo waziri masoud aliwasihi watendaji wa miondombinu na mfuko wa barabara  kuuboresha mfumo huo kwa kuingiza takwimu sahihi ili kuweza kutoa taarifa  sahihi kulingana na wakati pamoja na kuwawezesha watendaji  kuongeza ujuzi kulingana ba mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Barabara Abdi Khamis amesema
uanzishwaji wa mfumo wa RMMS zilianza takribani miaka miwili iliyopita
kwa kuanza na Wizara ya Miundombinu na mawasiliano kupitia mradi wa
Zanzibar road upgrading project.
 Hata hivyo  amesema mfumo huo umekuja wakati muafaka   ambapo  hivi sasa Zanzibar nayo itakuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea kama mfumo huo utatumika ipasavyo.
Mfumo huo umeandaliwa  kwa
mashirikiano makubwa ya kampuni ya ITECO Consult T ltd iliyoshinda
zabuni hiyo ya uandaaji wa mfumo huo ambapo imegharimu jumla ya TSH     207,000,000.00.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa