Home » » MOHAMED ABOUD MOHAMED AZUNGUMZIA MSWAADA WA SHERIA WA MFUKO WA JIMBO

MOHAMED ABOUD MOHAMED AZUNGUMZIA MSWAADA WA SHERIA WA MFUKO WA JIMBO


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar  

Waziri wa nchi Afisi ya makamu wapili  wa Rais Mohamed Abuod Mohamed amesema lengo la serilali ya Mapindunzi  ya
Zanzibar ni kuona kwamba wananchi wake wana fanikiwa katika masuala
mbali mbali ya kimaendeleo ili jamii iondokane na umasikini na kupiga
hatua  kiuchumi  katika majimbo yao .

Hayo
ameysema leo huko baraza la wakilishi wakati alipo kuwa akiwasilisha
Mswada wa Sheria wa kuazisha Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kupitia  wakilishi  Majmiboni.

Amesema hatua hiyo  ita wafanya wananchi kujikwamua na masula yanayo wakwaza kama vile maji ,umeme afya elimu  na mengineo. 

Amesema  hapo awali serikali ilikuwa ikisaidia majimbo kupitia  Wizara ya fedha  na uchumi kwenye miradi midogo midogo ambapo  kulijitokeza  kasoro kadhaa ikiwemo  wananchi  kudai kwamba misada hiyo ikitolewa bila ya utaratibu mzuri na kwa upendeleo .

Hivyo amesema  mfuko huo utaweza kuondo  kasoro hizo kwani  utakuwa chini ya uangalizi wakamati maalum zitazo washirikisha madiwani, masheha na waakilishi wa majimbo.

 Amesema mfuko kama huo umeonyesha mafanikio katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo Kenya  ambazo zimepiga hatua kubwa kimaendeleo. 

Naye
mwenye kiti wa kamati ya Barza la Wakilishi ya kusimamia Ofisi za
Viongozi wa Kuu wa Kitaifa Hamza Hssani Juma akiwasilisha Tarifa ya
kamati hiyo amesema  mfuko huwo kupitia sheria itayo pitishwa utasaidia kuondoa kero ndgo ndogo za wananchi  majimboni.

 Nadharia ya kuanzisha mfuko huo kunatokana na  Ziara ya kimasomo ya wajumbe wa baraza hilo  nchini Kenya mwaka 2008-9 kujifunza  jinsi ya  mfuko huo ulivyoweza kusaidia jimbo la Naivasha nchini Kenya..

Amesema
jimbo hilo lilifanikiwa sana katika sekta ya elimu,Barabara ,ujenzi wa
Gereza la Watoto na kusaidia ada za skuli kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa