Home » » Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu haiwezi kuvunja muungano CCM

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu haiwezi kuvunja muungano CCM







Na Thabit Jaha, Zanzibar.

Chama
cha Mapinduzi(CCM) kimesema Muungano hautavunjwa na Jumuiya ya Uamsho
na Mihadhara ya Kiislamu kwani Jumuiya hiyo haina mamlaka ya kuwaamulia
Watanzania hatma na mustakabali wao.
Onyo
hilo limetolewa na Jumuiya tatu za CCM katika mkutano wa hadhara
uliofanyika uwanja wa mabata Zanzibar ambapo iliweka bayana msimamo wa
Chama hicho kulinda Muungano na Mapinduzi kwa gharama yoyote.
“Sisi
tunawaambia Muungano hautavunjika kwa kisingizio cha katiba mpya,katiba
mpya ni sehemu tu ya mabadiliko ya kukuza demokrasia ya utawala…CCM
ikiwa zao la ASP na TANU tunawajibu wa kutetea historia yetu ya umoja na
mshikamano” Alisema Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya  Wazazi Taifa,  Ramadhan Abdallah Ali
Alisema
kumejitokeza kikundi cha watu wanaojificha kwenye mwamvuli wa Jumuiya
ya kidini kuandesha kampeni chafu za kusambaratisha Taifa la Tanzania
kwa kutumia mpango mkakati wa kutoa elimu ya uraia Visiwani Zanzibar na
kushangazwa na vyombo vya Dola kuwafumbia macho watu hao.
“Vyombo
vya Dola vinakaa kimya,viongozi wa Kitaifa wanatukanwa na kudhalilishwa
na kikundi hichi, haiwezekani watu wanachochea uasi dhidi ya
Jamhuri,lakini hakuna hatua zinazochukuliwa…CCM tunasema muda wa
kuwavumilia umekwisha” Alionya Mjumbe huyo.
Alisema kwamba  wanaopinga na kutaka kuvunja Muungano wa Tanzania pia wana lengo na mipango maalum ya  kusambaratisha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 ambayo yaliongozwa na ASP .
“Kwa
kweli tusifanye mchezo na uchochezi unaofanywa na watu hao, vikundi
kama hivi ndio vilianzisha vurugu katika Mataifa mbalimbali,leo mnasikia
kuna Al shabab,Boko- haram,Fisi na wengineo wote hao kabla walijificha
kwenye mwamvuli wa dini,hawa wa Zanzibar tumashawabaini, tuwakatae”
Alisisitiza.
Mkutano
huo umefanyika huku kukiwa na kundi lililoanzisha kampeni ya hadharani
kushawishi wananchi kukataa Muungano kwa madai kwamba haujaleta faida
kwa Wazanzibari.
Mbali na udini, pia kikundi hicho haikijitofautisha na vyama hasimu vilivyokuwa vikipinga Muungano ambapo  matamshi yao, vitendo na muenekano wao hauna tofauti na wapinga mapinduzi.
Katibu huyo mstaafu wa CCM Mkoa Mjini Magharibi amesisitiza kuwa  Mapinduzi
ya 1964 ndiyo yaliowaletea heshima na kutambuliwa kwa utu wao waafrika
wanyonge waliokuwa wakibaguliwa na kutumikishwa.
“Hakuna
mjinga yeyote hapa Zanzibar asiejua kuwa mpango wao si kueneza dini ila
ni kutaka kusambaratisha Mapinduzi,wao wanaelewa fika kuwa Muungano  huu hautavunjika milele kwasababu hawakuunda wao na wala hawatambui madhumuni ya nchi mbili hizi kuunganishwa ”Alisema Ali
Ali aliwakumbusha wananchi utawala wa Kifalme wa  Oman waliikalia Zanzibar kwa miaka 132 kwa kulindwa na Uingereza  wakichota
rasilimali ,kuwatumikisha na kuwabagua wananchi bila ya kufanyika kura
ya maoni ili kujua wananchi wangapi wanautaka ukoloni au wanaupinga.
Alitoa
mfano kuwa tangu kufuzu kwa Mapinduzi,Mfalme na aila yake, wapinga
mapinduzi walijaribu kutaka kuyaondoa mapinduzi ambapo jaribio kubwa ni
lile la kumuua Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,marehemu Abeid Amani Karume.
Alisema wana CCM na wazalendo wengine hususan  wanyonge wa Zanzibar wanajua kuwa wale waliopinduliwa hawakupenda kuondoshwa na hadi sasa bado wanaota na kutamani  kurejea kushika utawala.
 “Uamsho
msijifiche nyuma ya kivuli cha dini,uislam ni dini adhim na
tukufu,hakuna hata dini yoyote inayoelezea uvunjifu wa amani kwa
kuchochea utengano miongoni mwa  jamii, acheni kujifanya mnaeneza dini wakati mnafanya siasa” Alionya.
Akizundua
Tume ya Katiba,Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kwamba katiba mpya
haitavunja Muungano na kuwaonya watu wanaochochea suala hilo kuacha mara
moja.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa