Home » » nchi ya china na mikakati mikubwa ya kuisadia zanzibar.

nchi ya china na mikakati mikubwa ya kuisadia zanzibar.



Waziri wa Habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok akizungumza na Balozi mdogo wa China aliyeko Zanzibar Bibi Sheen Limun(mwenye fulana nyeusi) kuhusiana na maswala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuisadia Zanzibar. 
Picha na Hamad Hijja-Maelezo Zanzibar.



Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok ameiomba Serikali ya China  kuwapatia mafunzo waandishi wa habari na watangazaji wa Zanzibar ili yasaidiye kurahisisha majukumu yao ya kazi za kila siku katika sehemu zao.

Waziri Mbaruok ameyasema hayo leo huko ofisini kwake Kikwajuni mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi mdogo wa china aliyepo Zanzibar Bibi Sheen Limun ambapo wamebadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali.

Amesema kuwa wanahitaji msaada kutoka China ikiwemo kupatiwa mafunzo kwa waandishi wa habari wa hapa Zanzibar ambapo mafunzo hayo yatasaidia na kurahisisha utendaji wa kazi zao.

Aidha Akizungumzia juu ya suala la uwanja wa michezo wa Mao tsetunge Waziri  Mbaruok amesema kuwa uwanja huo una  jina kubwa kwa hapa Zanzibar lakini hali yake hailingani na jina lake na hivyo kumuomba Balozi huyo kuliangalia suala hilo kwa jicho la huruma

Waziri alisema kuwa muda mfupi ujao Zanzibar itaingia katika mfumo wa digital na kuachana na mfumo wa sasa wa analogia na hivyo kuiomba China iisaidie Zanzibar katika kukabiliana na mfumo huo mpya.

Aidha Waziri huyo wa habari ameitaka Jamhuri hiyo ya China kuongeza mashirikiano yao ya muda mrefu na Zanzibar na ambapo pia ametoa rai ya kuanzishwa kwa safari za kitalii baina ya China na Zanzibar.

Kwa upande wake Balozi huyo mdogo wa china Sheen Lemun amesema kuwa maelezo yote yaliyotolewa na waziri  anayehusika na habari,utalii,utamaduni na michezo Zanzibar ameyachukuwa na atayapeleka kunako husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi. 

Balozi Sheen akizungumzia juu ya suala la uwanja wa Mau Balozi amsema kuwa atatembelea katika uwanja huo ili aone hali halisi ya uwanja wenyewe na ikiwezekana waangaliye namna ya kutengeneza. 

Aidha Bibi Sheen Lemun amesema kuwa Serikali ya China itaipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ruzuku ya dolla million kumi ili ziweze kusaidia katika masuala mbali mbali yakiwemo ya utangazaji.

Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitakachotolewa na serikali ya china kinalenga kuisaidia Zanzibar kutumika kununuwa ving’amuzi Laki mbili ambavyo vitasaidia upatikanaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Zanzibar ZBC

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa