Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu kiongozi, DKT Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein amemteuwa Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Afisa Tawala wa Mkoa Mjini/Magharibi Unguja. Kabla ya Uteuzi huo Ayoub alikuwa Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti katika Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati.
Aidha Dkt Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Sahina Ameir Mwita kuwa Mkurugenzi wa Mipango,Sera, na Utafiti katika Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. Kabla ya Uteuzi huo Salhina alikuwa Afisa wa Mipango katika Wizara hiyo.
Pia Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Ardhi iliosajiliwa Namba 10 ya 1990, amemteuwa Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed kuwa Msajili wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati.
Kabla ya Uteuzi huo Mwanamkaa alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mashtaka Zanzibar.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
11/4/2012
0 comments:
Post a Comment