Home » » Maalim Seif akemea uchafuzi wa mazingira

Maalim Seif akemea uchafuzi wa mazingira


na Mauwa Mohammed, Zanzibar
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amekemea vikali kitendo cha baadhi ya  watu kuendelea kuchafua mazingira hasa katika vyanzo vya maji.
Seif alitoa onyo hilo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea vyanzo vya maji katika chemchemi ya Mtopepo Mjini Magharibi, akisema ni hatari kuona vitendo hivyo vikiendelea huku taifa likikabiliwa na uhaba wa maji unaotokana na uharibifu huo.
“Ikiwa vitendo hivyo vitaachiwa kuendelea, kuna hatari ya taifa kuwa na upungufu mkubwa wa maji katika miaka michache ijayo huku mahitaji ya maji yakizidi kuongezeka,” alisema Maalim Seif.
Hata hivyo, katika kudhibiti hali hiyo, alisema kuwa serikali itachukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha vvyazo vya maji haviendelei kuharibiwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa), Dk. Mustafa Garu, alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa ni uvamizi wa ujenzi karibu na vyazo vya maji, hali inayosababisha mfumo wa uzalishaji wa maji kubadilika na kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha maji katika chemchemi.
Naye Mhandisi wa Mamlaka hiyo, injinia Said Saleh, alisema baadhi ya chemchemi ndogo ndogo zimeanza kutoweka, na kutaka tahadhari zaidi zichukuliwe katika kudhibiti uvamizi wa vianzio hivyo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa