Habari Michuzi na Watanzania wote.
Ushauri wangu kwa Idara ya Uhamiaji Tanzania na hasa kwa Zanzibar.
Passport za Zanzibar zimekuwa zikitolewa bila kufuata ujwazaji wa fomu kwa ushahidi wangu mwenyewe na wa mwenzangu.Mfano .
1.Passport yangu ya Mwanzo imetolewa kwa Jina la MOH'D kwa kuwa Ulaya wanafuata kilichoandikwa "Name as appeared in the Passport or Travel document" kwa hiyo jina linajulikana ni MOH'D cha kushangaza Passport nilipoomba tena kutokana na uchakavu wa Pasi ya Zamani jina limeandikwa Mohamed kwa kirefu, sasa imepelekea kutokubaliwa kwa maombi ya ukaazi hadi wapate uthibitisho kuwa MOH'D ndio ile ile Mohamed process ambayo imechukua muda mrefu kutokana hatuna Balozi wala Consulate wa Tanzania au hata wa Africa anotuwakilisha.
Licha ya kuwa kuna Muhuri ndani ya Pasi kuwa passport ya zamani imekuwa Withdrawal/cancel/lost lakini nimeambiwa bado haitoshi kutokana kilichobadilika ni Jina, ilitakiwa barua ya mahakamani kuthibitisha hilo na form nilijaza kama Pasi ya zamani inavoonesha MOH'D.
Pili.Ushauri kwa VYETI VYA KUZALIWA NA VYA NDOA AU KARATASI ZA FAMILY STATUS NA NYENGINEZO zinazotoka Zanzibar,(sikusudii kuchafua mambo ya Muungano ila kuturahisishia tu kwa sasa) tungelipenda ziandikwe The United Republic of Tanzania,BADALA ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,hili ni tatizo kutokana Zanzibar haitambuliki na haimo kwenye Database zao sasa inatupata shida sana tunatakiwa tutengeneze vyeti vya TANZANIA na kwa Zanzibar sijui vinatoka wapi,wala Dar es Salaam sijui wapi vinatoka kwa hiyo ni bora mfumo uwe mmoja tu au angalau liandikwe neneo United Republic.
Ni hayo tu kwa kuwa hadi sasa hakijaeleweka inabidi nianze process mpya kufuatilia karatasi zote Tanzania hadi kupigishwa mihuri ubalozi na commonwealth pia translation na kufunga safari kwenda U.K kufuatilia.
Ahsante.
Mdau
ST.Helena
Kwa hisani ya Michuzi Blog
Kwa hisani ya Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment