Home » » UAMSHO ZANZIBAR WASALIM AMRI KWA POLISI

UAMSHO ZANZIBAR WASALIM AMRI KWA POLISI




Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar


Wananchi
wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kilichotangaza
kufanyika kwa mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba mjini hapa, kimetii
amri ya Jeshi la Polisi kwa kutoonekana kwa muumini ama viongozi wa
kikundi hicho katika viwanja hivyo.

Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
amesema leo kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali
ya mji wa Zanzibar na hivyo kutojitokeza tena kwa wafuasi wa kikundi
hicho kama ilivyotangazwa awali.


Inspekta
Mhina amesema Kikundi hicho cha Uamsho kupitia kwa Kiongozi wake
Sheikhe Farid Hadi, juzi kilijigamba kufanya Mhadhara mkubwa leo arasili
katika viwanja vya Lumumba mjini hapa hata baada ya Serikali kupiga
marufuku mikusanyiko, kimeshindwa kufanya hivyo kufuatia agizo la Jeshi
la Polisi lakuwataka wasitishe vinginevyo wangekabiliana na mkono wa
dola.


Jana
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Mussa Ali Mussa, alitangaza kuupiga
marufuko mhadhara huo na kuwataka wananchi na waumini kutohudhuria na
kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo angechukuliwa hatua kali.


Kufuatia
agizo hilo, Polisi wa Operesheni maalum leo, walimwagwa katika viwanja
vya Lumumba huku magari yenye askari wa kutuliza ghasia yakiranda kwa
kila eneo kumkabili yeyote atakayekaidi na kufika kwenye viwanja hivyo
kwa madhumuni ya kuhudhuria mhadhara huo.


Hatua
hiyo ya Polisi imeweza kudhoofisha kabisa hali ya majigambo ya viongozi
na wafuasi wa Kikundi hicho cha Uamsho waliotangaza kufanya mhadhara
huo hata baada ya serikali kupiga marufuku.


Viongozi
wa kikundi hicho ambao walionekana kugawanyika waliwajulisha baadhi ya
wafuasi wao kuwa hali isingekuwa swari kwa upande wao kutokana na Jeshi
la Polisi kusambaza makachero na askari wa kawaida katika maeneo
mbalimbali ikiwemo Viwanja vya Lumumba palipopangwa kufanyika kwa
mhadhara huo.
Ni
wafuasi wachache tu walionekana kufika katika msikiti wa Mbuyuni kwa
sala ya kawaida na pengine kupata taarifa za hatima ya mhadhara huo
uliopigwa stop na Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa