Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 01/08/2012.
Mwanasiasa Mkongwe Hassan Nassor Moyo amewataka wananchi wa Zanzíbar kuzungumzia suala zima la mustakbali wa nchi na sio kuchanganya mambo kwani nchi ni mali ya wananchi hivyo wanahaki ya kusikilizwa nini wanataka.
Amesema chama kinaweza kuwepo na kuondoka lakini nchi haiondoki hivyo wananchi wapewe fursa ya kuzungumzia suala la nchi yao na mambo wanayotaka kubadilishwa katika Muungano bila ya ugomvi wala fujo .
Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa Rumaisa karibú na Hoteli ya Bwawani wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo Mbali Mbali , wanafunzi wa chuo kikuu,pamoja na wananchi waliofika hapo .
“Siwezi kupinga Muungano hata mara moja lakini Muungano tuubadilishe,” alisema, Moyo .
Aidha alisema ili kuimarishwa Muungano ni lazima ufanyiwe marekebisho ya kasoro zinazojitokeza zirekebishwe kwa furaha na sio kwa chuki na jazba .
“Tuzungumzie muungano kwanza katiba mwisho , tunataka uhuru wa kujitawala wenyewe sio kutawaliwa,”alisema Moyo. Alidai kuwa wananchi wengi wanasema hawautaki Muungano uliopo hivi sasa wanataka muungano ambao utaendana na wakati uliopo.
Aidha alifahamisha kwamba kuna baadhi ya kasoro ambazo zilijitokeza kabla ya Marehemu Karume ziliambiwa kwamba kurekebishwa bado haijafika wakati wake sasa wakati ndio huu wakurekebisha kasoro hizo.
Hassan Nassor Moyo ambaye anatokea katika vyama vya Wafanyakazi Zanzíbar alishika nyadhifa Mbale Mbale katika Serikali ya Mapinduzi na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment