Home » » MWANASHERIA MKUU MPYA WA ZANZIBAR AAPISHWA BARAZANI

MWANASHERIA MKUU MPYA WA ZANZIBAR AAPISHWA BARAZANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, jana alimuapisha Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, Said Hassan Said, kiapo maalum cha uaminifu kwa Baraza hilo.
Baada ya kiapo hicho, Kificho aliwataka wajumbe wa Baraza kumpa ushirikiano ili atomize majukumu yake kwa ufanisi.

Alisema bila ya ushirikiano wa wajumbe hao, Mwanasheria huyo atashindwa kutekeleza majukumu yake ndani na nje ya Baraza hilo.

Kuapishwa kwa Said kunafuatia kuteuliwa kwake na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kufuta uteuzi wa Masoud Othman Masoud, September mwaka huu.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo walimpongeza Mwanasheria huyo kwa uteuzi wake na kuahidi kumpa ushirikiano ili kuweza kutimiza majukumu yake ya kazi.
 

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa