Tukio hilo ni la kukabidhi Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Taarifa iliyotolewa mjini humo jana na Kamanda wa Polisi Mkoa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), David Misime, alisema ulinzi huo unahusisha askari wanaofanya doria za miguu, magari, pikipiki, mbwa na farasi.
Alisema pia wameshirikiana na vyombo vyote vya dola katika kubadilishana taarifa mbalimbali na wote wako mitaani kufuatilia tukio hilo muhimu kwa kutumia mbinu zote walizonazo.
Kamanda Misime aliwahakikishia wakazi wa mkoa huo na wageni kuwa, usalama ni mkubwa, hivyo wanaomba ushirikiano pale watakapomtilia shaka mtu yeyote au jambo lolote kwa kuwajulisha polisi na wao watalifanyia kazi haraka.
“Wenye nyumba za kulala wageni, waimarishe ulinzi katika maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao, wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa,” alisema.
Aliwataka wananchi na wageni, watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu, atashurutishwa kwa e kwa mujibu wa sheria za nchi
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment