Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma Abdallah amewaahidi Viongozi, Watendaji, wanaCCM na wananchi kwa ujumla kuwa atasimamia kwa vitendo maendeleo, amani na mshikamano ndani na nje ya chama hicho.
Ahadi
hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa chama na
jumuiya zake mara baada ya kuwasili visiwani humu akitoka Dodoma ambapo
aliteuliwa kushikilia nafasi hiyo, ambayo awali ilikuwa chini ya Naibu
Katibu Mkuu Mstaafu Vuai Ali Vuai.
Dkt.
Juma alisema kuwa CCM Zanzibar itaendelea kuimarika endapo wanachama na
viongozi wa Taasisi hiyo ya kisiasa watazifanyia kazi kwa vitendo
falsafa za maendeleo na umoja kwa wote.
“ Nimekabidhiwa kijiti hiki ili niweze kuendeleza na kusimamia maslahi ya CCM Visiwani Zanzibar ambayo
mtangulizi wangu Nd. Vuai Ali Vuai na wengine waliopita kabla yake
wamefanya kazi kubwa ya kusimamia bila ya woga misingi ya maendeleo
ndani ya chama chetu, nami nitafuata nyayo hizo na kuongezea mikakati
mingine itakayosaidia kuongeza ufanisi.”, alisema Dkt. Juma maarufu
Mabodi huku akimsifu Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Vuai Ali Vuai kwa
utendaji na ukomavu wa kisiasa uliomjengea heshima na uaminifu mkubwa
ndani na nje ya chama hicho.
Akitaja
baadhi ya vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuishauri na kuisimamia
serikali iliyopo madarakani chini ya CCM, kuhakikisha inatatua
changamoto sugu zinazowakabili wananchi kwa baadhi ya mitaa na maeneo ya
pembe zoni.
Alisema
katika juhudi za kupunguza changamoto za ajira nchini serikali imeweza
kutekeleza mpango wa awamu ya tatu wa kuimarisha uchumi wa nchini kwa
kufungua milango ya wawekezaji kujenga viwanda ili vitoe ajira kwa
wazalendo.
Pia
alieleza kwamba mbali na mikakati hiyo bado serikali ina mipango
endelevu ya kuanzisha viwanda huru vya usindikaji wa samaki, kilimo cha
kisasa na kuimarisha miundombinu ya ndani.
Akitaja
mikakati ya kuimarisha utendaji wa chama hicho kuanzia ngazi za chini
alisema atahakikisha kila tawi na maskani za CCM zinawekewa masanduku ya
maoni ili wanachama waweze kutoa maoni yao na makatibu wa ofisi hizo
wayawasilishe kwa ngazi husika ili yafanyiwe kazi na ngazi husika.
Aliweka
wazi msimamo wake kuwa yeye sio muumini wa makundi ya kugawa na
kuharibu CCM , bali ni mtu anayependa kujumuika na watu wenye fikra na
mitizamo ya kimaendeleo na kiutendaji.
“
Naomba nisije kueleweka vibaya kwa hilo kwani itafikia wakati
nitaikosoa serikali kwa baadhi ya mambo ambayo naona hayaendi sawa kwa
wananchi ili yaweze kutekelezwa kwa haraka, japo najua kuna baadhi yetu
watasema nimekuwa mpinzani lakini ukweli ni kuwa natengeneza heshima ya
Chama na serikali iliyopo madarakani.”, alifafanua Naibu Katibu Mkuu
huyo.
Hata
hivyo aliwakumbusha baadhi ya viongozi watakaopewa jukumu la kusimamia
uchaguzi wa Chama unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ili kuhakikisha kila
mwanachama mwenye sifa na nia ya kugombea au kupiga kura anapata haki
hizo kidemokrasia.
Mapema
Naibu Katibu Mkuu mstaafu, Nd. Vuai Ali Vuai akimkaribisha Naibu Katibu
Mkuu huyo mpya Dkt. Abdallah Juma, aliwashukru wafuasi wa CCM, viongozi
na watumishi wa chama na jumuiya zote kwa ushirikiano wao pindi
alipokuwa katika utumishi wa taasisi hiyo.
Aliwataka ushirikiano huo uendelezwe kwa Naibu katibu Mkuu mpya ili kuimarisha maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ndani ya chama.
“
Nimekitumikia chama hiki zaidi ya miaka 36 hivyo nimejifunza mengi na
kupambana na changamoto mbali mbali lakini hakuna siku niliyorudi nyuma
bali nilisonga mbele bila ya kujali ni nani anayenikwaza na nikaishi kwa imani moja ya kulinda maslahi ya CCM popote.
Pia
kustaafu kwangu ni jambo la kawaida ndani ya CCM kwani wamepita
viongozi wengi kwa kupokezana madaraka, na huo ndio ukomavu wa kisiasa
na uimara wa Demokrasia uliopo ndani ya chama chetu, kwani hakuna
kiongozi wa kudumu madarakani.”, alisema Vuai Ali Vuai.
Kuteuliwa
kwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma
kunatokana na maamuzi yaliyofanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama
uliofanyika Dodoma hivi karibu pamoja na mambo mengine ulifanya
marekebisho katiba ya CCM ya mwaka 1977.
Dkt.
Mabodi kitaaluma ni Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji na utafti wa
maiti, ambaye amewahi kuhudumu nafasi mbali mbali zikiwemo Mkurugenzi
Mkuu wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Mwanzilishi wa Chuo cha madaktari wa
Cuba Zanzibar pamoja na nafasi mbali mbali zinazoendana na taaluma hiyo.
Taaluma
nyingine ni mtaalamu wa masuala ya Mikakati ya maendeleo Kimataifa,
nafasi iliyowahi kumpatia fursa ya unaibu Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki.
Kwa
upande wa siasa ni miongozi mwa vijana wa mwanzo wa CCM toka enzi za
Youth legue ambayo kwa sasa ni UVCCM na amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la
Rahaleo kabla ya majimbo hayo kukatwa upya.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment