NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
WAFUASI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamekishauri Chama hicho
kuweka masharti maalum kwenye mikataba ya miradi ya maendeleo
inayofungwa baina ya taasisi hiyo na wawekezaji kuhakikisha
wanazingatia matakwa ya kutoa ajira kwa vijana na makada wa Chama
hicho.
Walitoa
rai hiyo wakati wa ufungaji wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Vuai Ali Vuai ya kuimarisha taasisi hiyo ya kisiasa kuanzia
ngazi za mashina hadi Majimbo ya Mkoa wa Mjini Kichama huko Tawi la CCM
Malindi Jimbo la Mji Mkongwe Unguja.
Walisema
kuwa CCM na Jumuiya zake wana miradi mijini na vijijni inayotokana na
matunda ya urithi wa waasisi wa chama hicho toka enzi za ASP
inayotumiwa na baadhi ya wawekezaji wazalendo na kigeni ambayo
mikataba inayofungwa haiwataki wawekezaji hao kutoa fursa za ajira kwa
makada wa chama hicho.
Walishauri
kuwa wakati umefika wa kuhakikisha mikataba mbali mbali ya miradi ya
maendeleo ya CCM ikiwemo ukodishaji wa maduka, nyumba, rasilimali ya
ardhi na biashara zinawekewa masharti ya kutoa ajira kwa vijana ili
kupunguza kasi ya changamoto za upungufu wa ajira nchini.
Aidha
walikiomba chama hicho pindi panapojengwa matawi ya kisasa wasisahau
kulinda Matawi na nyumba za zamani ambazo ni urithi kutoka kwa
waasisi wa CCM ili zibaki kama sehemu ya historia kwa vizazi vya sasa
na vijavyo kufahamu asili ya chama hicho wapi kilipotoka, kilipo na
kinapoelekea katika zama za maendeleo kwa wote.
Akizungumza
katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai
aliwakumbusha Watumishi na viongozi wa Chama na jumuiya wa ngazi mbali
mbali kuwa wao ndiyo wanaotakiwa kuwa wa kwanza kuratibu changamoto
mbali mbali zinazowakabili wananchi hasa tatizo la ulinzi na usalama
kwa kuziwasilisha katika mamlaka husika zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
Aliwataka
Wanachama na viongozi wa ngazi za mashina, wadi, majimbo hadi Mikoa
kuhakikisha wanajianda kikamilifu kutekeleza matakwa ya ibara ya 14
(3) ya Katiba ya Chama hicho inayoelekeza haki ya Kila mwanachama
kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi wa ngazi mbali mbali za chama
hicho.
Vuai
alieleza kuwa Chama hicho kwa sasa kina mambo matatu ya msingi
yanayotakiwa kuwekewa mikakati ya kudumu ambayo ni kuingiza muundo mpya
wa chama katika Katiba, Uchaguzi wa CCM na hatimaye Uchaguzi Mkuu wa
Dola mwaka 2020.
Alisema
pamoja na mambo mengine kila mwanachama kwa nafasi yake anatakiwa
kuanza mapema kujiandaa kisaikolojia kwa kuwahamasisha wanachama wapya
wajiunge na CCM hasa wa vyama vya upinzani kwa lengo la kupata
wanachama wa uhakika watakaoweza kukichagua chama hicho katika Chaguzi
za dola zijazo.
Sambamba
na hayo aliwaagiza viongozi na watendaji wa Chama kuhakikisha
wanafuatilia kwa kina Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya
mwaka 2015/2020 inayotekelezwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed
Shein , Wabunge, Wawakilishi, serikali za mitaa na serikali kuu ili
kujiridhisha kama inatekelezwa vizuri kulingana na mahitaji ya
wananchi kama walivyoahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi.
“
Tusitosheke na taarifa za utekelezaji tunazoletewa kwa njia ya
makaratasi ama kuambiwa na viongozi na taasisi zetu zinazotakiwa
kutekeleza Ilani yetu bali tunatakiwa twende katika sehemu husika
kufanya tathimini na kuona uhalisia wa hiyo miradi ili kujua na kutafuta
ufumbuzi wa kushughulikia maeneo yenye changamoto sugu na kuwakumbusha
wahusika.”, alisema Vuai.
Hata
hivyo alisisitiza umoja na ushirikiano ndani ya ngazi mbali mbali za
taasisi hiyo na kuwaeleza kuwa endapo watakuwa wamoja hakuna chama
chochote kitakachoweza kuigawa CCM ama kuhujumu mikakati yake.
Alikemea
tabia ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotumia nafasi zao vibaya
kuwakosoa na kuwashutumu nje ya vikao halali hali inayotoa nafasi ya
kutengeneza fitna na majungu.
Pia
alisema kupitia mabadiliko ya kimuundo ya Chama hicho yamewataka
viongozi wa ngazi za juu za Chama na Jumuiya kuhakikisha wanashuka
ngazi za chini kwenda kufanya kazi na wanachama na kubaini changamoto
zilizomo katika taasisi hiyo.
Hata hata hivyo alienda mbali kwa kueleza kwamba mabadiliko hayo yataingizwa katika Katiba ya CCM kupitia Mkutano mkuu maalumu unaotarajiwa kufanyika Machi 12, mwaka huu mkoani Dodoma.
Alisema
Mkutano huo utakuwa wa kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Dk. John
Magufuli baada ya kupokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Jakaya
Kikwete.
Alisema
lengo la mabadiliko hayo ni kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya
Chama hicho sambamba na kupunguza gharama za kiutendaji kwa lengo la
kujenga uchumi imara wa chama na kuongeza kasi za kiutendaji kwa maslahi
ya wanachama na wananchi kwa ujumla.
“Mkutano
huu pamoja na mambo mengine utafanya kazi yakujadili na kupitisha
marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012, pamoja na
kanuni za chama cha mapinduzi na jumuiya zake,”alifafanua Vuai na
kuwambia wanachama hao pamoja na viongozi kuwa wasiwe na hofu kwani
mabadiliko hayo yanaendana na mahitaji ya Siasa za zama za Sayansi na
Teknolojia.
Naibu
Katibu Mkuu huyo akihitimisha ziara ya kuimarisha chama ndani ya Mkoa
wa Mjini kichama aliwapongeza viongozi, wanachama, watendaji na wananchi
kwa ujumla waliojitokeza kwa wingi katika vikao vyake na kutoa maoni,
mapendekezo na ushauri wao wenye malengo ya kutengeneza CCM mpya na
Tanzania mpya zenye nguvu imara kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Pamoja
na hayo Nd. Vuai alisema kwa niaba ya wanachama wa CCM Zanzibar
anawapongeza Mwenyekiti wa Chama hicho , Dkt John Pombe Magufuli pamoja
na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa
kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010/2020, hatua
iliyozaa matunda kwa muda mfupi toka waingie madarakani na kuwasihi
viongozi wa chama na serikali kufuata nyayo za viongozi hao walioijengea
heshima Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment